desktop logo

EXPLORE

DATA

twitterfacebook
mobile logo
news
Serikali ya Taita Taveta Yakoselewa kwa Ujenzi wa Daraja
April 2023
PesaYetu
article

Share

By Selestine Lunani

Wakaazi wa wadi ya Kaloleni  eneo bunge la Voi  kaunti ya Taita Taveta wametoa lawama kwa serikali ya kaunti kwa madai ya bajeti ya  shilingi milioni 2.7 iliyotumiwa kwa ujenzi wa daraja la Kaloleni ,huku  wakitaka serikali  ya kaunti kufichua ukweli wa  budgeti hiyo.

Kutokana na serikali kutoweka wazi bajeti ya muradi huo, wakaazi hawa wanatashwishwi ya kiwango hicho cha pesa kilichotumika kutokana na daraja hilo kuanza kuonyesha mianya ya kupasaka.

Haya yanajiri huku changamoto ikiendelea  kutolewa kwa serikali ya kaunti ya Taita Taveta kuhakikisha inapanua daraja la kuvuka mto wa Voi kutoka Kasarani kuelekea mji wa Voi ili kurahisisha zaidi usafiri wa wananchi wanapotaka kutafuta huduma mbalimbali ikiwamo za matibabu katika hosipitali ya rufaa ya Moi,sawa na usafirishaji wa bidhaa zao za shambani. 

Wakazi wa eneo la Kasarani hasusani wale ambao wanajihusisha na kilimo wakiongozwa na Dora Maghuwa wanasema japo daraja hilo liliweza kujengwa linastahili kupanuliwa ili kuruhusu uchukuzi ikiwamo wa bodaboda ili kuwawezesha wananchi kuafikia huduma wanazohitaji kwa wakati mwafaka 

Bi Maghuwa pia ameelezea kuwa daraja hilo halikujengwa kwa njia inayostahili kwa kile anasema linatiwa wasiwasi wakati mtu anapovuka 

Kadhalika wamepongeza ujenzi wa daraja hilo wakisema umewasaidia katika kuendeleza biashara zao kutokana na mazao ya shambani sawa na shughuli zingine za kila siku Wakati huo wanasema umesaidia wanafunzi wa shule kufika shuleni kwa wakati.

Aidha, lalama za wakaazi hao kuhusu kupanuliwa kwa daraja hilo kunajiri baada ya aliyekuwa waziri wa fedha na mipango katika serikali Leonard Langat kuelezea kupanuliwa kwa daraja hilo miaka mbili  iliyopita  ahadi ambayo hadi sasa haijatimizwa.

Haya yanajiri huku Kaunti ya Taita Taveta ikikadiria kuongezeka kwa ishara ya matokea katika sekta ya uchukuzi. 

Kwa upande wake gavana Graton Samboja uwepo wa daraja hii umesaidia sana wenyeji wa wardi ya kaloleni hasa wafanyi biashara na wakulima.

Image: Kaloleni footbridge. Source: Department of Public Works & Infrastructure -Taita Taveta County

Makala haya yameandaliwa na Mwanedu FM kwa kushirikiana na Code for Africa, Kenya Community Media Network (KCOMNET)  na Baraza la vyombo vya habari katoliki (CAMECO) kupitia msaada wa Ujerumani kama sehemu ya mradi wa kaunti yetu , jukumu letu.

Related Stories
Usambazaji wa Umeme Jijini Nairobi
By Sharon Gitonga Mkakati wa kuunganisha umeme ni swala ambalo lilipewa kipaumbele pindi tu serikali ya Jubilee ilipojinyakulia uongozi mnamo mwaka wa 2013. Mradi huu umeshuhudiwa kupanuka kwa kasi katika mji wa Nairobi. Sababu kuu  ni kumwezesha mwanachi wa kawaida kujimudu kimaisha. Kulingana na ripoti la CDIP,  jijini Nairobi, takribani asilimia tisini na tano ya […]
logo
This site is a project of Code for Africa, the continent’s largest network of civic technology and data journalism labs. All content is released under a Creative Commons attribution Licence 4.0. Reuse it to help empower your own community.

2022 PesaYetu

Resources
  • About
  • Privacy Policy
  • Terms of Service
Stay in touch with us
instagramfacebooktwitterlinkedin