Share
By Erick Mwangi
Maji safi na usafi wa mazingira ni lengo la maendeleo endelevu namba sita. Kutimiza lengo hili nchini, hatua kubwa zimefanywa ili kuhakikisha idadi ya wakaazi wa Nairobi wanapata maji safi huku wakizingatia usafi wa mazingira.
Mojawapo ya changamoto kuu katika kukuza mazingira ni udhibiti vya vyoo jijini licha ya maeneo kadhaa kutumia vyoo mbalimbali.
Kulingana na CDIP ya kati ya mwaka 2018 na 2022, idadi ya wakazi wanaotumia vyoo vya kusombwa ni 61.5%. Licha ya hayo, kaunti ya Nairobi imeweka mikakti kadhaa kuhakikisha wakazi wanapata vyoo dhabiti. Kwengineko kama njia ya kukuza mazingira, ripoti hii inaonyesha kuwa kaunti ilipanga kutenga kiasi kikubwa cha fedhaa kati ya mwaka wa 2018 hadi 2022.
Serikali ya jiji la imejenga vyoo vya umma katikati mwa mji ambavyo ni vya gharama ya chini.
Maji ikiwa ni kiungo muhimu, serikali ya jiji la Nairobi kupitia utendakazi wa mji NMS imeweka vituo vya maji safi katika mitaa ya mabanda kama vile Mkuru, Kawangware na maeneo mengine ambayo yamekuwa yakipitia changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hii muhimu.
Awali, wakaazi wa mitaa iliyoko eneo bunge la Dagoretti kama vile Waithaka, Konaa, Ngando na Gatina wamekuwa wakipitia changamoto ya kupata maji huku wakilazimika kununua bidhaa hii muhimu.
Kupitia NMS, wakazi hawa wanauwezo wa kupata maji safi siku tatu kwa wiki bila ya malipo.
Kwengineko, jitihada kadhaa zimefanywa kuboresha usafi wa mazingira kupitia upatikanaji wa vyoo vinavyoweza kusombwa na sehemu za kutupa takataka kwa ushirikiano na NMS.
Vilevile, NMS imeweza kutoa magari ya kukusanya takataka mara kwa mara. Kwa sasa, wakaazi wanaweza kutoa takataka maeneo yao ambayo husombwa kila siku.
Tangu mradi huo kuanzishwa, watu takribani 84,940 jijini Nairobi wanaweza kupata maji safi huku watu 13,7243 wakiwa na uwezo wa kutumia mabomba ya kupitisha maji taka.
Mradi huu umewasaidia wakaazi kupata vyoo vya kusombwa ambayo na kuchangia katika kuimarisha mazingira.
Image: A past Nairobi river cleaning exercise. Source: The Star.co.ke
Taarifa hii imeandaliwa na kituo cha Mtaani Radio kwa kushirikiana na Code for Africa, Kenya Community Media Network (KCOMNET) na Baraza la vyombo vya habari katoliki (CAMECO) kupitia msaada wa Ujerumani kama sehemu ya mradi wa kaunti yetu , jukumu letu.